info@mwakiautomobile.co.tz
"Low Mileage Cars at an affordable price"
Karibu Mwaki Automobile, tunafurahi kwa kutembelea tovuti yetu, sisi ni waagizaji wa magari toka kwenye masoko makubwa duniani wenye uzoefu na weledi katika tasnia hii, kwa hitaji lako lolote la magari toka ng’ambo tunapenda kukujulisha kuwa umefika sehemu sahihi maana huduma zetu ni bora sana na zenye kulenga ridhiko la mteja katika ubora, thamani, na muda wa wateja wetu. Pia, makubaliano yetu ni nafuu kwako na yenye kulenga kukufanikisha kwa wepesi zaidi.
Tutachambua pamoja katika masoko makubwa zaidi ya 20 yaliyoko nje ya Afrika ya Mashariki ili kuweza kupata chaguo lililo bora, chaguo lisilo na shaka na chaguo nafuu lakini lenye ubora usio na shaka na ambalo halitakutesa bali kuyafanya maisha yako ya barabarani kuwa ndoto njema iliyotimizwa
Huduma zetu ni za daraja la juu, tunapokuhudumia tunahakikisha tupo pamoja kwa mawasiliano yote utakayohitaji kwaajili ya kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi kila wakati ili kuweza kujibu maswali yako kwa vitendo mara zote unapohitaji kujibiwa
Kukusaidia kupata bidhaa bora yenye thamani inayoshabihiana na thamani ya pesa zako ulizovuja jasho kuzitafuta, hutajuta kamwe kuhudumiwa nasi maana tunathamini pesa zako na tusingependa upate hasara kwa kufanya machaguo yasiyofaa
Tunathamini wakati wako, huduma zetu zinakimbizana na muda uliopangwa tukijipa nafasi ya kuweza kukuhudumia kwa weledi na kukusaidia kufanikisha kuagiza gari uipendayo kwa wakati ili uweze kuendelea na mipango yako mingine
Tutatumia uzoefu wetu wa miaka isiyopungua kumi kukusaidia kupata gari imara, gari ambayo haitachoma pesa zako kila mara kwa matengenezo, gari itakayokufanya ufurahie kuwa nayo bila kukuingiza gharama zisizo za lazima
© Mwaki Automobile (T) Ltd
Design Silvanux | Afribrainy