send

info@mwakiautomobile.co.tz

MWAKI AUTOMOBILE CO.LTD

"Low Mileage Cars at an affordable price"

Huduma zetu

Katika mchakato wote wa kuleta gari ZURI na BORA kwa mteja, kampuni yetu inafanya ulinganisho wa hitaji lako moja katika masoko zaidi ya 20 huko nje, na kisha kushea na wewe au kuona kwa pamoja na kuchagua gari ipi tuilete kwaajili yako, miongoni mwa ambazo tutakuwa tumezichagua ili uchague moja wapo. Katika kupata kilichobora na kizuri kampuni yetu HAINA ukomo wa masoko gani tutanunua hitaji lako au hatutonunua hitaji lako kwa maana hiyo tutaweza kufikia makampuni mbalimbali huko Japan, Singapore, Dubai na UK pasipo miiko yoyote au pasipo kizuizi chochote. Yaani tutanunua na kulipia hitaji lako kutoka kampuni yoyote duniani inayouza bidhaa hizo.

Kwanini uchague huduma zetu?

Hatuna ukomo wa masoko, tuna zaidi ya masoko 20
Usalama wa fedha zako na mali yako, unafuu na uzoefu wa utoaji wa huduma husika
kupata gari yako ndani ya muda mfupi
kuokoa fedha kwa kuwa kwetu ni nafuu kuliko kwingine kokote
Uwazi wa huduma, kujua kila kitu kwa pamoja waziwazi, kitu kinachoelekea kupata hitaji (bidhaa) inayoendana na fedha yako (value for money)
Taarifa kiganjani mwako masaa 24 (muda wowote) kuhusu gari yako
Tumekuwa waaminifu na wenye misimamo ya kuleta gari nzuri, na zenye kilometa chache na kwa unafuu
Tunabeba dhamana ya kusimamia gari yako, hata kwenye ukaguzi wa ndani ya nchi kwa gari yako (siku hizi ukaguzi unafanyika ndani ya nchi).
Uzoefu na mahusiano mazuri kati yetu na wauzaji huko nje hufanya tupate punguzo kubwa kwaajili ya wateja wetu.
Huduma zetu ni endelevu na zenye ofa za kutosha kila siku mfano fire extinguisher, triangle, t-shirt, usajili pamoja na 'Bima bure' ni ofa ya muda wote.
Gari tunazochagua kwa niaba ya mteja tunahakikisha HAZINA wala HAZIFIKI nchini na KASORO yoyote ile.
Mapungufu yoyote yatakayojitokeza kwenye gari ya mteja kampuni itawajibika na suala hilo

Malipo

Malipo hufanyika kwa awamu mbili mpaka tatu tofauti tofauti, kuna malipo ya awamu ya kwanza na malipo ya awamu ya pili, lakini pia ukiweza kufanya kwa awamu tatu kadri uwezavyo ndani ya siku 45
i. Malipo ya awamu ya kwanza
Haya ni yale malipo ya awali ambayo hulipwa na mteja kwa mara ya kwanza anapokuwa amepata hitaji au chaguo lake la gari aliyoipenda
ii. Malipo ya awamu ya pili
Haya ni malipo yanayolipwa kumalizia balance ya jumla kuu ya gari aliyoiagiza na mara nyingi malipo haya hulipwa wakati meli yenye gari la mteja inapokuwa imefika kwetu (bandarini) na wanaolipa awamu zaidi ya mbili ni wale wanaopenda kulipa chochote kila wanapopata, wakati wanaendelea kusubiri gari yake kwa maana ya kulipa kwa kupunguza kidogo kidogo ndani ya mwezi na nusu (yaani ndani ya siku 45) malipo yote anayotakiwa kuyalipa mteja, hulipwa kwenye akaunti ya kampuni yenye jina la kampuni kwa maana ya MWAKI AUTOMOBILE CO LTD na si vinginevyo.

Wezeshwa na Mwaki

Programu ya WEZESHWA NA MWAKI ni programu yenye msaada kwa wale wanaopenda huduma ya kulipa na kuchukua gari papo hapo, japo ni utaratibu ambao kampuni imejiwekea kwa kuamua kuleta gari nzuri moja moja kila mwezi ili kuwauzia watu wasiopenda kungojea muda wa siku 45 kupata hitaji. Lakini hapa tofauti yetu na wenye showroom ni kwamba, kwanza, mteja anaweza kulipa tu asilimia 75 au 80 kisha kukabidhiwa gari ambayo itakuwa imeletwa na kutangazwa. Pili, mteja atapata muda wa kukagua gari tangu lilivyo sokoni huko lilipotoka na atakagua pia lilivyofika nchini ili tu kuondoa hofu juu ya ubora, lakini pia kuendelea kuwa wakweli kwa huduma zetu tofauti na wale wanaocheat specifications za gari husika. Tatu, mteja ndio anaweza kueleza juu ya muda gani atakuwa amemaliza kulipia fedha nyingine kukamilisha hesabu kwa muda wote ambao pia atakuwa na gari yake


Gereji popote

Mwaki Automobile pia tuna huduma ya gereji popote kwa msaada wa kutatua shida za gari yako na kukufikia popote ulipo ili kufanya matengenezo ya gari yako, unaweza kupiga simu kwa huduma hii hata kama unataka kufanyiwa service ya gari yako nyumbani kwako. Huduma hii kwa sasa inapatikana ndani ya jiji la Dar es salaam tu
Iwe issue ya kufanya service ya gari
Iwe issue ya mambo ya umeme wa gari yako
Iwe issue yoyote inayohusu chombo chako cha moto(gari) tuite tutakufikia na kutatua matatizo ya chombo chako kwa maana tuna mafundi wazuri mno.
KITU KINGINE KIZURI ni kwamba endapo gari yako itakuwa na matengenezo ya siku au ya muda mrefu, bado Mwaki Automobile tupo na wewe kwa kuweza kukupatia gari ya kutembelea kwa kipindi hicho cha matengenezo ya gari yako na ni kwa maelewano mazuri na gharama nafuu kabisa.


Bima kiganjani

Katika kuhakikisha unapata huduma BORA na SALAMA, pia tuna BIMA kwaajili ya gari yako.
Zaidi katika kutekeleza sheria na kanuni mbalimbali, tunahakikisha tunakuelezea kwa kina kila BIMA ili mteja upate kuelewa vizuri juu ya BIMA ambayo umechagua kuikatia gari yako.
Gharama za BIMA kwa miaka ya hivi karibuni zote zina kiwango sawasawa kilichopangwa na mamlaka husika ili kila kampuni au wakala wa bima kuwa na viwango sawasawa kulingana na thamani halisi ya gari ya mteja, hivyo, mwenye kuhitaji bima kubwa (comprehensive insurance) kama atatoa figure sahihi ya thamani ya gari yake kiasi cha fedha au malipo ya hiyo bima ya gari huwa sawasawa kwa mawakala wote.
Lakini kikubwa kinachotufanya sisi kuwa tofauti na wengine kwenye bima ni ile nidhamu ya kufuatilia FIDIA kwa mteja ambaye amepata huduma ya bima kutoka kwetu.


© Mwaki Automobile (T) Ltd

Design Silvanux | Afribrainy